Sunday, August 13

DED ILEJE AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA HALMASHAURI YAKE


Na Fredy Mgunda, Ileje: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi amefanya ziara ya kushtukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015/20 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya 
mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni 
wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6 wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawaugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mfereji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo.

Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yao.

Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo, alimwagiza mtendaji wa kata ya mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kuwa, kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani
 Songwe, Haji Mnasi akikagua mradi wa mfereji mkubwa
 wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa 
wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na
wananchi wakati wa ukaguzi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo walipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

"Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment