Friday, October 13

JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAZIWA



MAHITAJI
Maziwa ½ lita
Ngano 1 kilo
Mafuta
Chumvi kijiko kimoja cha chakula

JINSI YA KUPIKA
Bandika mafuta kiasi jikoni yaache yachemke halafu yamimine kwenye ngano, kisha koroga na mwiko au kijiko ili usiungue mikono.
Bandika maziwa jikoni na hakikisha yamechemka vizuri kisha yamimine kwenye ngano uanze kukanda unga wako taratibu.
Wakati ukikanda ongeza maziwa kama mchanganyiko wako bado mzito na endelea kufanya hivyo hadi uwe mwepesi.
Unga ukiwa tayari kata matonge halafu anza kusukuma chapatti kwa ajili ya kuchoma.
Wakati unachoma acha iive mpaka upate rangi ya kahawia, geuza upande wa pili na kuongeza mafuta kidogo huku ukiendelea kuigeuza geuza mpaka iive.
Baada ya kuiva ondoa na kuweka kwenye sahani safi na hadi hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Chakula hiki kinaweza kuliwa asubuhi kama kifungua kinywa au jioni sambamba na mchuzi wa nyama, maharagwe au supu ya samaki.

No comments:

Post a Comment