Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Octoba 30, imeahirisha kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi wa meno ya tembo ya bilioni 13 a raia wa China, Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' na wenzake wawili sababu, shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake leo anaumwa.
Mwendesha Mashtaka wa serikali, Wankyo Simon amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini shahidi anaumwa, akaomba ipangiwe tarehe nyingine.
Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alisema hana pingamizi na kesi hiyo imeahirishwa hadi November 7 mwaka huu.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.
Washtakiwa hao, wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.
Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
No comments:
Post a Comment