MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo imekataa kupokea msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka kama vielelezo vya ushahidi dhidi ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya imayomkabili Wema Sepetu na wenzake.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro.
Akitoa uamuzi wake amesema anakubaliana na hoja zilizotolewa na upande wa mashtaka kwamba msokoto wa bangi na vipisi hivyo vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.

Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na wafuasi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati wakisubiri kusomewa Mashtaka yanayomkabili ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na Wakili wake Peter Kibatara wakiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza mashtaka yanayo mkabili ya kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Wakili Peter Kibatara na Kushoto ni Mama wa Wema Sepetu.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa nche ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayo Mkabiri.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na wakili wake Peter Kibatara wakiwa nje ya Mahakama ja Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment