Monday, October 9

WAZIRI WA NISHATI, WAZIRI WA MADINI NA MANAIBU WAZIRI WAO WARIPOTI RASMI OFISI ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki, pamoja na Manaibu Waziri wa Wizara hizo wameripoti rasmi katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Ofisi hizo, Mawaziri hao  walifanya kikao cha pamoja ili kufahamishana masuala mbalimbali. Kikao hicho kiliwahusisha pia  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi, Juliana Pallangyo.

Aidha,  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walifanya  kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

Viongozi hao wanaosimamia Sekta ya Madini, wanatarajia kufanya kikao na watumishi wa Wizara husika tarehe 10 Oktoba, 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu walikutana na Wafanyakazi wa Wizara husika na kutoa maagizo mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati na hasa upatikanaji wa Umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia), Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa pili kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwa kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika (hawapo pichani )katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa kwanza kulia),  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

No comments:

Post a Comment