Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi (kulia).
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipata maelezo ya vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Mapango ya Amboni kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia vivutio mbalimbali vya maumbo asilia ikiwemo ya wanyama na alama za kuabudia vilivyomo ndani ya mapango hayo.
Muoneshaji wa Kujitolea katika Mapango ya Amboni, Othman Mangula (kulia) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii moja umbo la asili lenye taswira ya Chui ndani ya Mapango ya Amboni ambapo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii ndani ya mapango hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Dkt. Iddi Mfunda (kulia) na Muwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Canisius Karamaga (wa pili kulia) wakiangalia baadhi ya vivutio katika mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akipenya kwenye njia nyembamba iliyopo ndani ya mapango ya Amboni.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAOD_qzxR1lkQflt2S0QEFCDo6Q78qwJ5PwTJYXZH9WV_7Iad2uIFP7ve2kocMfAlyYLabhyphenhyphenE_CUu16OmoZjWGat87avePE0uaacIDPKayeXLqBi5p4rYkcPzHDtoh_v_IgC3YUPXrtO2t/s640/DSC_1506.JPG)
Moja ya umbile la asili lililojitengeneza ndani ya mapango ya Amboni likiwa na taswira ya kwato za ngo'mbe.
Maumbo mbalimbali ya asili yenye taswira ya viumbe ni moja ya kivutio kikubwa ndani ya mapango ya Amboni, Pichani ni umbo la asili lenye taswira ya matiti ambalo lipo ndani ya mapango hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akimsaidia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungu Ardhi, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya kushuka katika moja ya mteremko uliopo ndani ya mapango hayo.
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Canisius Karamaga akifurahia jambo ndani maporomoko hayo.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Alan Kijazi akiwa ndani ya mapango hayo.
Picha na; Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii
No comments:
Post a Comment