Thursday, November 9

JAMII YATAKIWA KUACHA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA KULETA MAENDELEO


MBUNGE Wa viti maalum Mkoa Wa Iringa, Ritta Kabati ametoa wito kwa jamii kuondoka na itikadi za kisiasa pindi linapokuja suala la maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza na wazazi na walezi wa shule ya msingi Igeleke wakati wa ukarabati wa madarasa ya shule hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni ahadi yake ya kukarabati shule za msingi zenye miundo mbinu mibovu na zamani, Kabati alisema kuwa suala la ujenzi wa madarasa hauna siasa.

Alisema kuwa maamuzi ya kukarabati shule za msingi lengo ni kuyaweka mazingira bora ya kusomea wanafunzi na kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uchakavu wa majengo.Kabati alisema kuwa imekuwa kawaida pindi mtu akitaka kufanya maendeleo mambo ya siasa yanaingizwa ila kwa serikali hii ya hapa kazi lazima tufanye kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa maamuzi kufanya shughuli za kijamii hasa katika elimu ni kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyo bora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo kama ilivyo kanda za Kaskazini ambapo elimu ni kipaumbele cha kwanza.

“Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi na kuondoa kasumba ya watu wengi wafanyakazi wa ndani ni kutoka mkoani hapa”alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule.Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi walio tayari kuleta maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo”
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akikabidhi saruji kwa uongozi wa shule kabla ya kuanza ukarabati katika shule ya msingi Igeleke.

No comments:

Post a Comment