Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Rais hao wawili wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wakiwa katika kijiji cha Luzinga, jirani na mpaka wa Mutukula.
Pia wamefungua kituo cha forodha chenye huduma zote muhimu kurahisisha safari kati ya nchi hizo mbili.
Rais Magufuli anafanya ziara Uganda kwa siku tatu.
Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000. Bomba linatarajia kukamilika mwaka 2020.
Mradi huo utakao gharimu dola za kimarekani bilioni 3 unajengwa kwa ushirikaino wa serikali za nchi hizo mbili na washirika na unatariji kutoa ajira zaidi ya 30,000.
No comments:
Post a Comment