Yamkini watu 13 wameuwawa kaskazini mwa India, baada ya ghasia kutokea, mara baada ya mahakama moja nchini humo, kumhukumu Guru mmoja anyemiliki dhehebu lake na anayejiita mtu mzuri, kwa kosa la kuwabaka wanawake.
Idara ya polisi inasema kuwa baadhi ya waumini wa mtu huyo wanaodaiwa kufikia milioni moja, walianzisha ghasia ya kuwarushia polisi kila aina ya silaha ikiwemo mawe, mara tu mahakama ilipotoa hukumu nhiyo.
Duru kutoka mji wa Panchkula zinathibitisha kuwa watu hao 13 kweli wamefariki, huku wawili wakiwa katika hali mahututi.
Hii ni kwa mjibu wa taarifa kutoka makao makuu ya Polisi katika jimbo la Panchkula, kaskazini mwa India.
Awali kulikuwa na hofu ya kutokea fujo, baada ya kiongozi huyo wa kidini:- Gurmeet Ram Rahim Singh, alipopatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono waumini wake wawili wa kike, katika kesi hiyo ya mwaka 2002.
Kisa hicho kinadaiwa kufanyika katika makao makuu ya kiongozi wa kundi hilo la Dera Sacha Sauda, iliyoko katika mji wa Sirsa, Kaskazini mwa India.
No comments:
Post a Comment