Saturday, September 16

WANASOKA,WASANII BONGOFLEVA WAUNGANA KAMPENI YA UZALENDO KWANZA

KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu nchini, a.k.a Bongo Muvi inazidi kupanua wigo wake baada ya kuongeza matawi yake kwa mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama wakongwe waliowahi kutamba ndani ya Soka hapa nchini. 

Akizungumza na wanahabari wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama hicho, Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa, lengo la Chama hicho ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi yako ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kumuunga mkono wa kizalendo katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo. 

"Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya Taifa,na Wasanii wetu wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza nchi yao kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere. 

Wacheza soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa Kihwelo, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.Aidha Nyerere amewaasa wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo vyao mfano, kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi. 

Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, atambulikae kwa jina la Ruby pia amejiunga na kampen ya Uzalendo Kwanza,Msanii huyo amepewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.

Katika hatua nyingine,Uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu Laki tano kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.

Steve Nyerere amemaliza kwa kuwaasa Wasanii wenzake kuendelea kuwa Wazalendo na kuwakumbusha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii,amesema kuwa mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni yao ya Uzalendo Kwanza,huku wakionesha utayari mkubwa wa kuwasaidia iwapo wataamua kuendelea kujiunga katika mfuko huo na ukawa mkombozi kwao.
Mmoja wa Mabalozi wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza akiwasili kwenye mkutano,Athuman Hamis aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News), ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimkabidhi bahasha yenye kiasi cha fedha shilingi laki tano pamoja na msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimnyanyua Mzee Rajab Shabani mkazi wa Mburahati ambaye ni mlemavu wa miguu (kwa miaka mitano sasa),kumkalisha kwenye kiti cha matairi matatu (Wheel chair),ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Wadau wa kampeni hiyo wakishirikiana na uongozi wa kampeni ya Uzalendo kwanza. 
Pichani kati ni Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,wakati akiwapokea wanachama wapya walioamua kujinga na kampeni hiyo.Pichani kulia ni Mjumbe Halima Yahya na kushoto ni Misayo Ndumbagwe. 
Pichani kati (njano) Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiwatambulisha wanamichezo wazalendo wa zamani katika Soka na Waigizaji wengie mahiri mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,walioamua kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
Pichani Kati ni Msanii wa bongofleva Hellen Majeshi a.k.a Ruby ambaye pia ametangazwa kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza. 

Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini Dar.

No comments:

Post a Comment