Pia imetoa maboksi mawili ya maziwa ya unga. Msaada huo unatokana naombi la JKCI kwa mashirika mbalimbali kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha huduma kwenye taasisi hiyo.
Dk Tulia Ackson, ambaye ni mwanzilishi wa taasisi ya Tulia amesema msaada wa runinga utawasaidia watoto kujifunza mambo mbalimbali na kupata burudani.
"Watoto wanapokuwa hapa muda mwingi wanawaza ugonjwa, lakini ikiwa wataangalia runinga watakuwa na muda wa kujifunza hesabu na mambo mengine kupitia vipindi na kuangalia katuni.Hata wazazi wataweza kuangalia taarifa za habari kujua nini kinaendelea," amesema.
Dk Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amesema, "Kumekuwa na shida katika kuwachangamsha watoto kutokana upungufu wa wafanyakazi na bajeti hairuhusu kununua vifaa hivi."
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema amefurahishwa na msaada huo na kukaribisha wadau wengine wajitokeza kuchangia nguvu ambazo Serikali inaweka katika kuboresha huduma za afya katika taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment