Monday, August 28

Kimbunga Harvey: Watu 2,000 waokolewa kutoka kwa mafuriko Houston, Marekani

Maafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyakeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyake
Watu takriban 2,000 wameokolewa kutoka kwa mafuriko katika mji wa Houston na viunga vyake, huku kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa sana maeneo ya jimbo la Texas.
Kumekuwa na ripoti za kutokea kwa vifo pamoja na magari kadha kuzidiwa na nguvu za maji.
Hata hivyo, uchunguzi bado unaendelea, afisi ya liwali mkuu wa wilaya ya Harris, Darryl Coleman amesema.
Gavana wa Texas Greg Abbott ameambia wanahabari kwamba hawezi kuthibitisha vifo vinavyodaiwa kutokana na mafuriko hayo.
Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali ambayo inashuhudiwa katika eneo hilo haijawahi kushuhudiwa awali.
Idara hiyo imesema kulitokea mafuriko ya ghafla eneo la katikati mwa mji wa Houston, na uchukuzi umetatizika.
Vyumba vingi vya kutoa hifadhi wakati wa majanga vimefunguliwa, ukiwemo ukumbi mmoja wa mikutano.
Gavana Abbot amesema barabara karibu 250 zimefungwa Texas na kwamba ameiomba serikali kuu itangaze janga katika wilaya 19, ombi ambalo limeidhinishwa na Rais Donald Trump.
"Tutaendelea kupokea mvua kubwa," amesema gavana huyo.
Flooded downtown Houston is seen from a high rise building along Buffalo BayouHaki miliki ya pichaTWITTER/@CAROLEENAM/REUTERS
NWS awali walisema walikuwa wamepokea taarifa za vifo vitano, lakini wamesema wameweza kuthibitisha kifo cha mtu mmoja pekee eneo la Houston.
Kufikia sasa, watu wawili wamethibitishwa kufariki tangu kimbunga hicho kilichofika maeneo ya bara, katika wilaya ya Aransas, ambapo Rockport ndio mji mkuu, mtu mmoja alifariki baada ya nyumba yake kushika moto Ijumaa usiku.
Na eneo la Houston, mwanamke mmoja alifariki akiendesha gari katika barabara zilizokuwa zimefurika maji Jumamosi.
Meya wa Houston Sylvester Turner amewashauri wakazi kutopigia simu maafisa wa huduma za dharura ila tu iwapo maisha yao yanatishiwa na wanahitaji kuokolewa kwa dharura.
"Msiingie barabarani. Msifikirie kwamba kimbunga kimepita," amesema.
Mjini Washington, ikulu ya White House imesema Rais Trump atazuru Texas Jumanne kutathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho.
Bw trump alikuwa amesema awali kwamba angezuru eneo hilo haraka iwezekanavyo lakini kwa kuhakikisha kwamba hatatatiza juhudi za uokoaji.
A vehicle partially submerged by floodwaters in HoustonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa wa hali ya hewa wamesema vifo vingi hutokea magari yanaposombwa na maji
Hurricane Harvey August 27, 2017 in HoustonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHouston ni moja ya miji yenye watu wengi zaidi Marekani
Kufikia saa nane adhuhuri saa za Texas Jumapili, NWS walisema mji wa Houston ulikuwa umeandikisha mvua ya kina cha sentimeta 64.8 (inchi 25.50) kwa mwezi Agosti, na kuufanya kuwa mwezi wenye mvua kubwa zaidi katika historia ya mji huo.
The path of Harvey

No comments:

Post a Comment