Monday, August 28

TAARIFA YA MKEMIA WA SERIKALI

SAMPULI YA MKOJO WA MASOGANGE UNACHEMBECHEMBE ZA DAWA ZA KULEVYA.


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imepokea taarifa ya mkemia wa Serikali iliionesha kwamba sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald "Masogange" una chembechembe za dawa za kulevya.

Mahakama imepokea sampuli hiyo kama kielelezo namba moja kwa cha ushahidi upande wa mashtaka ambapo baada ya pingamizi la upande wa lilitokuwa likitaka kisipokelewe kutupiliwa mbali

 Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali.

Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani.
Ameongeza polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.
Kesi imeahirishwa kwa muda.
.........UP DATES........
Shahidi namba mbili katika kesi hiyo, mpelelezi kutoka kituo cha polisi cha Kati, WP Judith ameieleza mahakama kuwa  alishuhudia Masogange akitoa sampuli ya mkojo kwa kuwa alisimama mlangoni.
Amedai kuwa alipewa chupa ya plastiki yenye namba ya maabara 446/2017 na kumuelekeza Masogange jinsi ya kufanya ambapo alipata sampuli ya mkojo huo.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, amedai Februari 15, mwaka huu aliitwa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai amchukue mshitakiwa Masogange na kumpeleka kwa Mkemia wa Serikali ambapo yeye akifuatana na Askari Polisi, Sospeter pamoja Masogange walienda kwa mkemia na kwamba saa 7 mchana walifika.
Akihojiwa na Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza ambaye alimtaka shahidi huyo kueleza  alikabidhiwa na nani chupa hiyo na kwamba mkojo ulikuwa na rangi oshahidi alieleza kuwa ulikuwa na rangi ya njano mpauko.
Kesi hiyo itaendelea Agosti 31, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment