Japan karate Association/World Federation - Tanzania (JKA/WF-TZ), ni shirikisho la mchezo wa karate wa asili ya Japani tawi la Tanzania, lenye usajili wa kimataifa toka makao makuu ya shirikisho hilo Tokyo Japan na pia hutambuliwa na Shirikisho la Karate la Dunia (World Karate Federation). JKA/WF-TZ ilipata usajili rasmi mwaka 2006, na ilishafanya semina na mashindano mengi ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Hivi sasa shirikisho lina timu ya Taifa ya karate inayojindaa na mashindo ya Afrika mwakani (2018), Mashindano ya Dunia (2019), Mashindano ya Olympics (2020), na pia mashindao mengine ya ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuendelea na maandalizi ya Timu ya Taifa sisi (JKA/WF-TZ) tunarajia kuendesha Mafunzo ya Karate na kufanya mitihani ya Kimataifa (International Karate Seminar & Grading ama Gasshuku), yatakayofanyika katika ukumbi mkubwa wa Don-Bosco Upanga, kuanzia tarehe 1-4 Septemba 2017. Saa 6:00 Mchana hadi saa 9:00 Alasiri.
Mafunzo na Mitihani hiyo itaongozwa na Mkufunzi (Master) Shihan Koichiro Okuma, kutoka Makao Makuu ya JKA Tokyo Japan, ambaye aliendesha mafunzo kama haya mwaka jana mwezi wa tisa, eneo lile lile la Don-Bosco Upanga. Mafunzo haya yatajumuisha nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kati, zikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zimbabwe, Zambia, DRC, Angola, Afrika Kusini, Ufaransa, nk. Hadi sasa mataifa ya Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Angola, Afrika kusini na Japan, yameshawasili nchini kuhudhuria mafunzo haya. Na tunatarajia kupata wageni wengi zaidi kadri muda unavyosogea.
Katika mafunzo hayo tunatakuwa na sherehe za ufunguzi siku ya kwanza (tar 1/9/2017 ) na sherehe kubwa siku ya mwisho (tar 4/9/2017) ambapo watahiniwa waliofuzu mafunzo watakabidhiwa vyeti na leseni zao siku hiyo ya mwisho, na wahudhuriaji watakabithiwa vyeti. Katika sherehe hizo, tunatarajia kuwa na Mgeni Rasmi toka BMT ambaye ni Katibu Mkuu, Bwana Mohamed kiganja. na pia tutakuwa mgeni toka Ubalozi wa Japani nchini.
Faida za ujio wa Shihan Koichiro Okuma (Toka Japan) na kuendesha mafunzo haya nchini:
Kwanza kama Taifa, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu (Tanzania) kimataifa kutokana na wageni wanaokuja kutoka nje na kwenda kusambaza habari zetu huko kwao, pia kuangaziwa na vyombo vya habari vya kimataifa, hasa katika suala na michezo, utalii nakibiashara.
Pili sisi kama JKA/WF-Tanzania, tutaongeza ujuzi kwa Wakufunzi/Walimu (Instructors), Waamuzi (Judges) wa Wachezaji (Karatekas) wa huu mchezo hapa nchini. Pia Shihan Okuma ataangazia matayarisho ya timu yetu ya Taifa inayojiandaa kwa mashindano ya Afrika mwakani (2018), mashindano ya Dunia (2019) na mashindano ya Olympics (2020). Sisi JKA/WF-Tanzania tutatumia fursa hii kuvuna mbinu mbinu mabalimbali za kushinda mashindano ya kimataifa na namna kuindaa timu kisaikolojia na kimwili/kimazoezi pia, katika hali ya kiutaalam zaidi.
Wenu katika michezo,
Nestory Fedeliko (FEDE)
Katibu Mtendaji, JKA/WF-Tanzania.
No comments:
Post a Comment