Wanamgambo wa Islamic State wametoa kile kinachoonekana kuwa ni kanda ya sauti ya kiongozi wa kundi hilo, Abu Bakr al-Baghdadi.
Mzungumzaji aliye na sauti kama ya kiongozi huyo wa IS anasikika akitaja tishio la hivi karibuni la Korea kaskazini dhidi ya Japan na Marekani.
Anazungumzia pia vita vya kupigania ngome za IS kama Mosul, mji uliodhibitiwa upya na vikosi vya Iraq mwezi Julai.
Baghdadi,ambaye anasakwa hajaonekana mbele ya umma tangu Julai 2014 jambo lililozusha uvumi mkubwa kuhusu hatma yake.
Mwisho alipoonekana alikuwa anatoa hotuba katika mskiti mkubwa wa al Nuri mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo na kulitangaza kuwa eneo wanalo litawala.
Aliopulizwa kuhusu kanda hiyo ya sauti, msemaji wa vikosi vya Marekani vinavyopigana na IS, Ryan Dillon, amesema "pasi kuwepo ushahidi wa kuthibitishwa wa kifo chake, tumeendelea kuamini kwamba yuko hai".
- Huenda kiongozi wa Islamic State bado yuko hai
- IS walipua msikiti wa kihistoria nchini Iraq
- Abu Bakr al-Baghdadi yuko wapi?
Msemaji wa idara ya ulinzi ameiambia BBC: "tunahafahamu kuhusu kanda hiyo ya sauti inayodaiwa kuwa ya Abu Bakr Al-Baghdadi na tunachukua hatua kuikagua.
Wakati hatuna sababu ya kuwa na shaka ya uhalisi wake, hatuwezi kuithibitisha kwa hivi sasa."
Kundi la wanamgambo wa kiislamu IS, lilitambulika kwa ghasia dhidi ya raia na wafungwa, limesukumwa nyuma Iraq na Syria mwaka huu.
No comments:
Post a Comment