Monday, August 14

DC Kibaha acharuka, atangaza kufuta hati za viwanja 1,000


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ametanga dhamira ya kufuta hati miliki za viwanja zaidi ya 1,000 vinavyomilikiwa na taasisi mbalimbali  zikiwemo benki na Idara za Serikali pamoja na watu binafsi wilayani humo.
Mshama alisema Serikali imedhamiria kufanya hivyo kwa sababu  wamiliki wake wameshindwa kuyaendeleza maeneo yao na kufanya mji huo kuzungukwa na vichaka na mapori  hivyo kusababisha kuenea vificho na matukio ya wahalifu.
Mshama amebainisha kuwa walishawakumbusha mara nyingi wahusika lakini kwa zaidi ya miaka mitatu sasa bado hawayaendelezi na hivyo yupo tayari kwenda mahakamani kutetea maendeleo ya Kibaha.
Ametaja idadi ya viwanja vilivyotelekezwa na kuwa mapori ni 1,080 ambapo kwa Kibaha mjini pekee ni viwanja 345 na Kibaha vijijini 735 huku kati ya hizo za taasisi na kampuni pekee ni 37.
"Hawa wote wamenunua ardhi Kibaha wametelekeza wameenda kujenga mikoani, hapa sisi wanatuachia vichaka na mapori na wahalifu wamegeuza maficho  hii haikubaliki, natoa siku 30 kila mwenye eneo aje aseme ana mpango gani sasa maana baada ya muda huo kama ajajenga tunafuta hati zao tunawapa wengine wenye nia,"alisema Mshama.

No comments:

Post a Comment