Monday, August 14

Mashamba 14 yafutwa Morogoro


Rais John Magufuli amefuta mashamba pori 14 yaliyokuwa yanamilikiwa na watu mbalimbali akiwemo mke wa waziri mkuu wa zamani Fredirick Sumaye na mfanyabiashara Jitu Patel.
Akitoa taarifa ya kufutwa kwa mashamba pori hayo kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi alisema kuwa mashamba hayo yamefutwa kutokana na wamiliki wake kushindwa kulipa kodi ya  ardhi na kuyaendeleza.
Lukuvi aliwaonya viongozi wanaotaka kujipenyeza kuchukua maeneo kwenye mashamba hayo na hivyo kumtaka mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya kusimamia kikamilifu zoezi la ugawaji wa maeneo ya mashamba hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amewataka wananchi kutovamia mashamba hayo yaliyofutwa badala yake wasubiri utaratibu wa kuyagawa.

No comments:

Post a Comment