Monday, October 2

Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza



Picha Na 1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida.
Picha Na 2
Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani).
Picha Na 3
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani)
Picha Na 4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
Picha Na 5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Picha Na 6
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
Picha Na 7
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho
…………………

Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani  Singida.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017  wamefanya  kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema  maandalizi hayo ni  juhudi za Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta  Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na  Eyasi nchini Tanzania.

Dkt. Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa husika.

Amesema wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.

“ Sisi kama  Tanzania  tupo  tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja;  hata hivyo pia tupo  tayari kubadilishana nao uzoefu  kwenye masuala ya  gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema  Dkt. Kalemani.

Ameongeza kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na kiongozi  wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na  Tanzania.

No comments:

Post a Comment