Mzee wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wanahudhuria tamasha ya muziki na kuwaua watu zaidi ya 58. Watu wengine 515 wanauguza majeraha.
Mshambuliaji alijipiga risasi, polisi wanasema.
Kulitokea nini?
Watu takriban 22,000 walikuwa wanahudhuria tamasha ya muziki wa country usiku wa Jumapili katika eneo la wazi karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Las Vegas.
Milio ya kwanza ya risasi ilisikika mwendo wa saa nne usiku saa za Las Vegas (05:00 GMT).
Mshambuliaji aliwafyatulia watu risasi kutoka ghorofa ya 32 katika hoteli ya Mandalay Bay na baadaye akajiua kwa kujipiga risasi.
Taarifa za awali zilikuwa zimesema kuwa aliuawa na polisi.
Walioshuhudia wanasema mamia ya risasi zilifyatulia na kwamba walisikia milioni ya bunduki za rashasha.
KuliZbuka mtafaruku na watu walikimbia huku na kule uwanjani wakijaribu kujificha.
Polisi wanasema kwamba taarifa kuwa kulikuwa na ufyatuaji wa risasi katika maeneo mengine ya uwanja wa ndege wa Las Vegas zilikuwa za uongo.
Mshukiwa ni nani?
Polisi wamesema wanaamini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 ndiye aliyehusika.
Hata hivyo, hawajasema chochote kuhusu nia ya mauaji hayo.
Mkuu wa polisi Joe Lombardo amesema maafisa wa polisi walipata hadi bunduki 10 katika chumba chake.
"Hatujapata maelezo yoyote baada ya uchunguzi au maelezo kumhusu mhusika huyo ambayo ni ya kukera (au kudokeza angetekeleza uhalifu)," Lombardo amesema.
"Jambo pekee tunaloweza kusema ni kwamba alitajwa katika kisa kimoja miaka michache iliyopita na kisa hicho kilishughulikiwa kama kisa cha kawaida katika mfumo wetu wa mahakama."
Maafisa wanaamini amekuwa hotelini humo tangu 28 Septemba.
Kakae Eric Paddock ameambia Reuters kwamba: "Hatuna habari zozote (kuhusu nia). Tumegutuka sana. Tumeshangazwa sana na tunatuma rambirambi zetu kwa jamaa za waathiriwa."
Kundi linalojiita Islamic State limedai kuhusika lakini halitajoa ithibati yoyote.
"Mshambuliaji huyo wa Las Vegas alisilimu miezi michache iliyopita," kundi la Islamic State limesema kupitia taarifa.
Kumetolewa wito wa kutafutwa kwa "mhusika mweingine" kwa jina Marilou Danley, 62, ambaye maafisa wanasema alikuwa anasafiri na mshambuliaji kabla ya kisa hicho kutokea.
Mwanamke huyo anaaminika kuwa alikuwa amesafiri nje ya Marekani.
Ni watu wangapi wameuawa?
Waliofariki wamefikia zaidi ya 58, kwa mujibu wa polisi.
Watu 515 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha.
Watu 14 wanaaminika kuwa katika hali mahututi, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
What has the president said?
Katika kituo na wanahabari White House, Rais Donald Trump amesema mauaji hayo ni "kitendo cha uovu".
Amewapongeza pia polisi wa Las Vegas kwa kuzuia mauaji zaidi, akisema walichukua hatua upesi sana.
Awali, rais huyo aliandika kwenye Twitter kuhusu shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment