Saturday, November 25

Kanzi Data Ya Kuhifadhi Taarifa Za Wadau Wa Tasnia Ya Filamu Kuleta Maslahi Katika Tasnia


Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga akielezea namna kampuni hiyo itakavyohifadhi data za wanatasnia ya filamu wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akifafanua jambo wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (wapili kushoto waliokaa) pamoja na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (katikati waliokaa) wakisaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Waliosimama katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kulia) akikabidhiana mkataba na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Wadau wa tasnia ya filamu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiunga katika vyama vilivyopo chini ya Shirikisho la filamu ili waweze kuingia katika mpango wa Kanzi Data inayolenga kuhifadhi taarifa za wasanii na kuinua maslahi ya tasnia kupitia tuzo na mashindano mbalimbali yatakayoandaliwa.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa kusaini mkataba wa kanzi data itakayohifadhi taarifa za wasanii wa filamu kati ya Kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.

“Ni wajibu wetu kuhamasisha wadau wa tasnia ya filamu kuingia katika mfumo wa kanzi data kwani mpango huu umedhamiria kuboresha na kuendeleza maslahi ya tasnia ya filamu na kuleta maendeleo ya msanii mmoja mmoja” amesema Mhe. Mwakyembe

Awali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa tasnia ya filamu imekua ikikosa fursa nyingi kutokana na wadau kutokua katika kanzi data inayowatambua vizuri hivyo ujio wa kanzi data hii utakua mkombozi kwa tasnia.

Bibi. Fissoo amesema kuwa suala la kanzi data limilikiwe na wadau wote kwa kupata uelewa na kila litakalofanyika katika kanzi data hiyo lifanywe kwa maslahi ya sekta ya filamu kwani filamu ni uchumi, filamu ni ajira na filamu ni kwa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga amesema kuwa kampuni yake inaingia mkataba wa kuunda kanzi data ya wanatasnia ya filamu na shirikisho la filamu kwa ajili ya kuongeza msukumo wa kuifanya tasnia ya filamu kukua na kuendelea kwa kasi zaidi.Aidha Bw. Mwasaga amesema kuwa kanzi data hiyo itasaidia kujua mapato yanayopatikana kupitia kazi za filamu lakini pia namna tasnia ya filamu inavyochangia katika pato la taifa.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa mchakato wa kufanikisha kanzi data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu unahitaji wanachama wasiopungua laki tano kwa kuanzia, na wanachama hao ni lazima wawe ndani ya vyama vilivyopo chini ya shirikisho la filamu huku kila mwanachama atakayekuwepo katika kanzi data hiyo atatakiwa kuchangia shilingi elfu moja kwa kila mwezi.

No comments:

Post a Comment