Watu nchini Liberia wanapiga kura kumchagua mrithi wa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa Rais barani Afrika na mshidi wa tuzo la amani la Nobel, Ellen Johnson Sirleaf.
Aliyekuwa mcheza kandanda nyota George Weah, na makamu wa rais Joseph Boakai ndio wagombea wakuu kwenye kinyanganyiro hicho.
Liberia, nchi iliyobuniwa na watumwa walioachiliwa huru kutoka Marekani karne ya 19, haijakuwa na mabadiliko ya amani ya madaraka kwa kipindi cha miaka 73.
Bi Sirleaf aliwashauri watu kupiga kura kwa amani kwenye taifa hilo ambalo bado linajijenga kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14.
"Kura yako inakuhusu wewe na familia yako, sio chama wala kabila," alisema Sirleaf wakati akihutubia taifa.
Jumla ya wagombea 20 wa urais wanawania urais kumritjhi Bi Sirleaf.
Wao ni pamoja na Alex Cummings, mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Coca-Cola na MacDella, mwanamitindo na mpenzi wa zamani wa Bw Weah.
Bi Sirleaf, 78, anaondoka madarakani baada kuongoza kwa mihula miwili.
Aliingia madarakani mwaka 2006 baada ya mtangulizi wake Charles Taylor, kulazimishwa kuondoka madarakani na waasi mwaka 2003.
Taylor kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makosa yanayohusu uhalifu wa kivita na mzozo katika nchi jirani ya Sierra Leone.
Bwana Weah, 51, amemteua mke wa zamani wa Taylor Jewel Howard, kama mgombea mwenza.
Hili ndilo la jaribio la tatu la George Weah kuwania urais.
Bi Sirleaf amishindwa kumfanyia kampeni Bw Boakai na kuzua uvumi kuwa wawili hao huenda wametofautiana.
Karibu watu milini 2.2 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Uchaguzi wa bunge nao unafanyika leo.
No comments:
Post a Comment