Tuesday, October 10

Raila Odinga ajiondoa kwa kinyang'anyiro cha urais Kenya

Kiongozi wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi, Kenya, Sept. 26, 2017.
Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tikiti ya muungano wa National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga, Jumanne alitangaza rasmi kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha marudio ya uchaguzi uliotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba
Odinga aliyatangaza hayo alipowahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi.
Haya yamejiri wakati wabunge wa mrengo wa upinzani wakisusia vikao vya kamati ya bunge kuhusu azma ya ubadilishaji wa sheria ya uchaguzi.
.Miswada hiyo iliyowasilishwa na wabunge wa chama tawala cha Rais Uhuru Kenyatta, iwapo itapitishwa katika viwango vyote na kuwa sheria, katika kura ya Urais ijayo, tume ya uchaguzi itatakiwa kutangaza matokeo ya kura hiyo sambamba kupitia mfumo wa kielektroniki na mfumo usio wa kielektroniki kutoka vituo vyote vya upigaji kura
Na iwapo mifumo hiyo miwili itatofautiana, mfumo usiokuwa wa kielektroniki ndio utakaoidhinishwa. Vile vile, matokeo ya kura hiyo hayatabatilishwa iwapo mfumo wa kielektroniki haukutumika kutangaza mshindi.
Hata hivyo upinzani, wakilishi wa makanisa pamoja na mabalozi wa nchi za kigeni wameonekana kujitenga na mswada huo.

No comments:

Post a Comment