Tuesday, October 10

NAIBU WAZIRI AWESO AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI UBUNGO



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.

Katika maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.

Naibu Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.

“Nitakaa na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.
 Fundi wa DAWASCO akiendelea na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.

No comments:

Post a Comment