Watu nchini Australia wamejitokeza kumtetea waziri mkuu Malcolm Turbull baada ya picha yake akimshika mjukuu wake na bia mkononi kuzungumziwa kwa wingi,.
Bwana Turbull alisambaza picha hiyo mwenyewe akimshika mjukuu wake kwenye uwanja mmoja wa kandanda mjini Sydney siku ya Jumamosi.
Picha hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Lakini ilizua maoni ya kumkosoa Bw Turnbul kutokana na kuwepo kwa bia.
- Waziri mkuu wa Australia aunga mkono ndoa ya jinsia moja
- Pacha waliotungwa siku tofauti Australia
- Kijana aumwa tena na buibui uumeni
"inakera kushika mtoto na bia mkononi," aliandika Marg Walker.
Suala hilo lilipata maoni mengi wakati lilianza kuangaziwa na vyombo vya habari.
Baada ya lawama kuibuka pia wale waliomtetea nao walinza kutoa maoni yao wakisema kuwa Bw. Turnbull hajafanya lolote baya.
No comments:
Post a Comment