KATIKA jitihada za kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya Utalii Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshughulikia Masuala ya wanyamapori na utalii wamepitisha mkakati wa kutangaza utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea leo na wandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema onyesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama kila mwaka.
Amesema kwa kutambua utalii ni sekta mtambuka onesha hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha uhifadhi wa maliasili na malikale pamoja na kuchochea ukuaji wa utalii hususani utalii wa mikutano na matukio (MICE TOURISM) ambao ni zao jipya la utalii la kimkakati la kufanikisha kuongeza idadi ya watalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
"Napenda kuwajulisha kuwa Tanzania ndio itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho hili la utalii wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kauli mbiu ya onesha hilo inasema " Utangazaji utalii stahimilivu kwa maendeleo jumuishi ya kijamii na uchumi, ".
Onesho la EARTE litafanyika jijini Arusha Oktoba 2021 ambapo litajumuisha siku tatu za maonesho na siku tano za ziara maalum ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii wa ndani kwa Tanzania bara na Zanzibar," Amesema Naibu Waziri Masanja.
Akizungumzia jinsi ugonjwa wa Corona ulivyoathiri sekta ya utalii ambapo kabla ya ugonjwa idadi ya watalii walifika Milioni 1.5 lakini baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo idadi ya watalii ilipungua na kufikia 620,000 huku makusanyo na mapato yakishuka.
" Kwa sasa hali inaenda vizuri baada Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kuleta chanjo ya ugonjwa wa Corona ambapo namba ya watalii kuingia nchini inapanda," amesema Naibu Waziri Masanja.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mary Masanja akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo alipokua akitangaza juu ya kuanza kwa onesho la utalii kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment