Monday, July 24

YANGA YAENDELEA KUJIFUA UWANJA WA UHURU


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kikosi cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo  Mzambia George Lwandamina.

Yanga waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki  moja na nusu ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.

Leo mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.

Mechi ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
 

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
 Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake  katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
 Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Kocha George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment