Afisa forodha msaidizi wa TRA, akitoka katika mahaka ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri ya kimiliki mali nyingi kuliko kipato chake.
Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
Afisa Forodha msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi leo October 24, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kukutwa akimiliki mali isiyolingana na kipato chake halali ambapo ni magari 19 ya aina tofauti.
Mshtakiwa huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Jennifer amesomewa hati ya mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wa mahakama hiyo.
Wakili Peter akisoma hati ya mashtaka amedai, kati ya Machi 21 na Juni 30 mwaka jana, jijini Dar es Salaam mshtakiwa Jennifer akiwa ameajiriwa na TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19 ya aina mbali mbali
Magari hayo yalitajwa kuwa ni, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota RAV4, Toyota Wish na Toyota Mark X.
Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry ambapo yote yanathamani ya Sh 197, 601, 207/- Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.
Katika shtaka la pili imedaiwa, kati ya Machi 21 ,2012 na Machi 30, mwaka jana jijini Dar es Salaam, Jennifer alikutwa akiishi maisha ya kifahari yenye thamani ya Sh 333,255,556.24/- fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.
Mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja atakayeweka bondi ya milioni 20.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Imeahirishwa hadi Novemba 7 kwa ajili ya kusikilizwa maelezo ya awali.
No comments:
Post a Comment