Wanawake wawili wanaokabiliwa na mashtaka ya kumuua Kim Jong-nam ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini wamepelekwa eneo la mkasa nchini Malaysia.
Siti Aisyah raia wa Indonesia na Doan Thi Huong raia wa Vietnam walipelekwa uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur leo Jumanne.
Wawili hao wanalaumiwa kwa kumwekea kemikali hatari ya VX Bw. Kim usoni wakati alikuwa anasubiri kuabiri ndege.
Wamekana mashtaka hayo ya mauaji wakisema kuwa walidanganywa kuwa kilikuwa ni kipindi cha runinga na majenti wa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imekana kuhusika kwenye mauaji hayo ya tarehe 13 Februari, lakini wanaume wanne wanoaminiwa kuwa raia wa Korea Kaskazini walioikimbia nchi siku ya mauaji nao wameshtakiwa.
Uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur ulifurika waandishi wa habari leo Jumamanne.
Baadaye wanawake hao wakafikishwa uwanja wa ndege wakiwa wamevalishwa mavazi yasiyopenya risasi.
Walisindikizwa na polisi wengi waliokuwa wamevaa mavazi yasiyopenya risasi
Ikiwa watapatikana na hatia wanawake hao wanakabiliwa na hukumu ya kifo. Mawakili wao watajaribu kuwatetea kuwa wahusika wakuu ni maajenti wa Korea Kaskazini ambao waliondoka Malaysia.
No comments:
Post a Comment