Ni mwaka sasa, tangu kufikishwa mahakamani kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lakini upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh 1.16 bilion inayowakabili bado haujakamilika.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakama ni hapo kwa Mara ya kwanza Agosti 18,2017.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hiku wakili Leornad Swai kutoka Takukuru, akidai kuwa jalada la kesi hiyo lililokuwapo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka DPP limekwisha rudishwa.
Hakimu Mwijage aliwaeleza upande wa Mashtaka wakamilishe upelelezi wa kesi hiyo ili washtakiwa kama walikula fedha za umma wafungwe kama hawajala waachiwe, siyo kula siku upelelezi haujakamilika maana yake nini.
Hakimu Mwijage aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6,2017 na kuutaka upande wa,Mashtaka siku hiyo uje na kitu na siyo upelelezi bado haujakamilika.
Mbali ya Maimu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.
Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 1,169,352,931
No comments:
Post a Comment