Gazeti moja la Marekani limeandika kuwa, washauri sita wa karibu wa rais Trump wamekuwa wakitumia barua pepe binafsi kuzungumzia masuala yahusuyo Ikulu ya Marekani tangu rais Trump kuingia madarakani.
Gazeti la New York times limeyataja majina ya washauri hao na mtoto wake Ivanka ni miongoni mwao.
Huku jalada la "Newsweek"lenyewe limeandika kuwa barua pepe alizokuwa anazitumia Ivanka alikuwa anatafuta ushirikiano na makampuni ya kibiashara na aliwatumia nakala wakuu wawili wa ofisi.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, rais Trump alitishia kuwafunga wapinzani wake pale ambapo Hillary Clinton alipotumia barua pepe yake ya binafsi wakati alipokuwa katibu wa serikali ya Marekani.
Na siku ya jumapili, mume wa Ivanka, Jared Kushner alitajwa pia kutumia barua pepe yake binafsi kuwasilisha shughuli za serikali.
Gazeti moja la Marekani limeandika kuwa, washauri sita wa karibu wa rais Trump wamekuwa wakitumia barua pepe za binafsi kuzungumzia masuala yahusuyo Ikulu ya Marekani tangu rais Trump kuingia madarakani.
No comments:
Post a Comment