Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akizungumza na baadhi ya wakazi wa Bunju A mapema leo asubuhi,waliokuwa Wakimsubiri Kumueleza Changamoto zao Mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya soko la wa Wafanyabishara wa soko la Bunju A ambalo inaelezwa kuwa limechukuliwa na Muwekezaji.
DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Wananchi hao,ikiwemo changamoto ya eneo la Soko Bunju A,Mh Hapi amesema ametoa siku kumi 14 kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi, huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo amepewa siku tatu kuwasilisha nyaraka zake za umiliki.
DC Hapi akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali,ambapo pia ametoa siku kumi 14 kwa ofisi ya Mkurugenzi kumletea nyaraka za soko la Bunju A ili ajiridhishe na kutoa maamuzi ya umiliki wa soko hilo kwa wananchi huku kwa mmiliki anayetajwa kuhodhi eneo hilo ametoa siku tatu ampelekee nyaraka zake za umiliki
Baadhi ya Wakazi wa Bunju A wakimsikiliza DC Hapi alipokuwa akizungumza nao mapema leo na kusikiliza matatizo ya wananchi hao ikiwemo pia kuyapatia majibu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi akisoma baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wakazi hao wa Bunju A mapema leo asubuhi,yakiwa na jumbe za changamoto zao wakihitaji kutatuliwa
No comments:
Post a Comment