Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.
Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.
No comments:
Post a Comment