Wednesday, October 25

Chama cha siasa kumlipa Eminem dola 412,000 kwa kutumia wimbo wake bila ruhusa

Rapper Eminem performs Not Afraid at the 2010 BET Awards in Los Angeles, 27 June 2010Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWimbo Lose Yourself ni moja ya nyimbo maarufu zaidi za Eminem
Chama kimoja cha siasa nchini New Zealand kimeamrishwa na mahakama kulipa dola 412,000 kwenye kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki raia wa Marekani Eminem.
Chama cha National Party, kilitumia mdundo wenye sauti sawa na wimbo wa Eminem wa Lose Yourself, katika matangazo yake ya uchaguzi.
Wimbo huo kwa jina Eminem-esque ulikuwa na tofauti kidogo na wimbo wake Eminem.
Kesi hiyo iliyoanza mwezi Mei ndiyo ya hivi punde kuhusu midundo inayofanana na muziki halali.
Wachapishaji wa nyimbo za Eminem Eight Mile Style, walipeka kesi mahakamani baada ya chama cha National Party, kutumia mdudo wa wimbo huo ulioshinda tuzo ya Oscar katika kampeni yake mwaka 2014.
Mawakili wa chama walisema kuwa mdundo uliotumiwa haukuwa wa wimbo wa Lose Yourself, lakini wimbo unaojulikana kama Eminem-esque, ambao waliununua kutoka maktaba ya muziki.
Hata hivyo mahakama iliamua siku ya Jumatano kuwa mdundo huo ulifanana na wimbo wa Eminem.

No comments:

Post a Comment