Thursday, October 19

SAA 24 BAADA YA KUJIUZULU KWA JACKSON MAYANJA, SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA MRUNDI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga.
Akitoa utambulisho huo mbele ya  waandishi wa habari,  Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda.

Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani.

“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili  mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.
Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana.
“Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma.

Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia  Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”
Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.
Afisa habari wa Simba Haji Manara akimtambukisha kocha mpya Masoud Djuma (Kulia) aliyechukua nafasi ya Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya wa Simba Richard Robert leo katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. 


No comments:

Post a Comment