Baada ya sauti ya Tundu Lissu kusikika kwa mara ya kwanza akizungumza kutoka Nairobi, mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amempa ushauri. Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu atulie hadi apone kabla hajasema mengi. Soma: Nape aeleza alichoambiwa na Lissu wakitoka bungeni jana Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ya leo Alhamisi akiwa ameambatanisha na picha ya Lissu ameandika, “Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la matumaini! Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi! Tulia mjomba upone kabisa kwanza!”
No comments:
Post a Comment