Thursday, October 19

Mahakama kutoa uamuzi wa pingamizi kesi ya Mdee, Bulaya


Dodoma. Mahakama Kuu Oktoba 30,2017  itatoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na upande wa Serikali katika maombi ya wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa
kosa ya kudharau kiti cha Spika.
Wabunge hao waliosimamishwa katika Bunge la bajeti Juni, 2017 ni Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini.
Mdee na Bulaya wamefungua mashtaka
katika Mahakama Kuu wakidai uamuzi huo umekiuka Kanuni za Bunge na Katiba.
Katika kesi hiyo leo Alhamisi Oktoba 19,2017 mawakili wa wabunge hao, Jeremia Mtobesya na Fred Kalonga wameiomba Mahakama iwaelekeze Spika wa Bunge au Katibu Bunge wawapatie taarifa walizoomba na kutoa ruhusa ya kuzitumia.
Wakili Mkuu wa Serikali, Angaza Mwipopo aliyewasilisha pingamizi kwa hati ya kiapo amedai wabunge hao hawakutumia fursa zingine walizonazo kabla ya kufungua shtaka hilo mahakamani.
Jaji Awadhi Mohamed aliyesikiliza pingamizi hizo ameahirisha maombi hayo akisema uamuzi atautoa Oktoba 30,2017.

No comments:

Post a Comment