Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao walikamatwa juzi Oktoba 17,2017 katika stendi kuu ya mabasi mjini Urambo.
Amesema waliokamatwa wanaume ni wawili, wanawake watano na watoto 14 ambao walitokea Kigoma na walikuwa wakitafuta usafiri wa kwenda mjini Tabora.
Kamanda Mutafungwa amesema leo Alhamisi Oktoba 19,2017 kuwa watu hao walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasiri.
“Hawajasema walikuwa wakitaka kuelekea nchi gani lakini wanadai wamekimbia machafuko nchini kwao na wanatafuta kambi ya wakimbizi kwa ajili ya hifadhi,” amesema.
Kamanda Mutafungwa amesema watu hao ni kutoka familia tano zenye watu wanne, saba, watatu, sita na nyingine mmoja.
Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa polisi wanapowashuku wahamiaji haramu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Mutafungwa ameema polisi inashirikiana na Idara ya Uhamiaji katika kushughulikia suala wahamiaji hao.
Mmoja wa watu hao, Dieudonne Buloze akizungumza kwa lugha ya Kiswahili amesema walisafiri kwa njia ya maji hadi nchini sehemu wasiyoijua na kuingia Tabora.
“Tumekimbia mapigano kati ya Serikali na waasi na tunataka kuwa kwenye makambi ya wakimbizi,” amesema.
Watu hao walipewa chakula baada ya kulalamika kuwa wana njaa.
No comments:
Post a Comment