Seneta wa chama cha Republican aliyekuwa wakati mmoja mgombeaji wa Urais, John McCain, amesema kuwa atapiga kura kupinga mpango wa chama chake wa kufutilia mbali bima ya wagonjwa iliyoanzishwa na Rais Barack Obama ijulikanayo kama ObamaCare.
Alisema kuwa moyo wake haumruhusu kuunga mkoto upigaji marufuku wa bima hiyo inayowasaidia watu wa mapato ya chini bila kuwa na takwimu za kuonyesha watakaonufaika na watakaoathirika.
Mbali na Bwana McCain, seneta mwingine mmoja wa Republican amesema kuwa anapinga ufutiliaji mbali wa bima hiyo.
Tayari wengine wawili wametangaza kuwa wanapinga mswada huo wa chama cha Republican.
Kwa kuwa vyama vikuu viwili katika bunge la Seneti linashindiana wanachama wachache sana ni dhahiri kuwa mswada huo hautapita.
Rais Trump ametumia mtandao wa Twitter kumkosoa yeyote anayepinga kuangamizwa kwa bima ya ObamaCare.
Hata hivyo wafadhili wa mswada huo wanasema wataendelea kuusukuma siku zijazo hadi wafaulu.
No comments:
Post a Comment