Saturday, September 23

Trump na Kim Jong-Un waitana ''wenda wazimu''

Rais Kim Jong Un na mwenzake wa Donald TrumpHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais Kim Jong Un na mwenzake wa Donald Trump
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ''na matatizo ya kiakili'' yamempatia motisha zaidi ya kuendelea kutengeza makombora ya taifa lake.
Katika taarifa ya kibinafsi isio ya kawaida, bwana Kim amesema kuwa rais Trump ''atalipia kauli'' zake za hotuba ya baraza la Umoja wa mataifa ambapo alionya kuiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujilinda.
Bwana Trump naye alijibu akisema kuwa ''mwenda wazimu'' hajawahi kufanyiwa atakachofanyiwa akijaribu.
Mataifa hayo mawili wamejibizana kwa kurushiana maneneo makali katika siku za hivi karibuni.
Rais Kim alimaliza taarifa yake kwa kusema kwamba atamnyamazisha kiongozi huyo ''aliye na akili punguani'' kwa vita.
China ilijibu vita hivyo vya maneno ikionya kuwa hali ni mbaya.
''Pande zote zinafaa kujikaza badala ya kuchokozana'' , alisema msemaji wa waziri wa maswala ya kigeni Lu Kang.Urusi pia ilitoa wito wa kuvumiliana .
Msemaji wa ikulu rais Dmitry Peskov alisema kuwa Moscow ina wasiwasi kuhusu kiwango cha wasiwasi kinachozidi kuongezeka.
Korea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake katika kiwango kisicho cha kawaida na kufanya jaribio lake la sita la kinyuklia licha ya shutuma za kimataifa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini Ri Yong -ho ambaye awali alikuwa ameifananisha hotuba ya rais Trump kama ile ya ''mbwa anayebweka'' ameonya kuwa Pyongyang italifanyia jaribio bomu lake la H-Bomb katika bahari ya pacific kujibu tishio la rais Trump.
''Bomu hilo litakuwa bomu lenye uwezo mkubwa kuwahi kurushwa katika bahari hiyo ya pacific'' , Bwana Ri alisema akinukuliwa na shirika la habari nchini Korea Ksakzini Yonhap.
Hatahivyo, aliongezea: Hatujui ni hatua gani zitachukuliwa na rais Kim jong-un

No comments:

Post a Comment