Saturday, September 23

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

China yaiwekea vikwazo Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionMagari ya kubeba mafuta kotoka China Kueleka Korea Kaskazini
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.
Rais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifa
Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kazi katika sekta hiyo nchini Korea Kaskazini.

No comments:

Post a Comment