Saturday, September 23

Mawakili wa Uingereza wamtaka Magufuli kuanzisha uchunguzi kuhusu Lissu

Rais John Pombe Magufuli
Image captionRais John Pombe Magufuli
Chama cha mawakili na watetezi wa haki za kibinaadamu nchini Uingereza wamemuandikia rais John Pombe Magufuli kikimtaka kuanzisha uchunguzi ulio huru mara moja kuhusu jaribio la mauaji lililotekelezwa dhidi ya mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu.
Wakili huyo ambaye pia ni rais wa chama cha mawakili nchini Tanzania TLS mnamo tarehe 7 mwezi Septemba alipigwa risasi tumboni na miguuni na watu wasiojulikana katika makaazi yake ya Dodoma.
''Ufyatulianaji huo wa risasi na maswala mengine ambaye yemetokeo yanayowahusisha mawakili yanatia wasiwasi''.
Ni muhimu mkubwa kwamba chama cha mawakili kinaheshimiwa kwa kuwa ni kitengo muhimu katika kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa kikamilifu, ilisema barua hiyo.
Hali ya mbunge Tundu Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi Dodoma wiki iliyopita
Barua hiyo ilisainiwa siku ya Jumatano na rais wa chama cha mawakili Joe Egan ,mwenyekiti wa baraza hilo Andrew Langdon na Mmwenyekiti wake Kirsty Brimelow.
Mawakili hao wamemwambia rais Magufuli pia kuanzisha uchunguzi kuhusu visa vyengine vya uhalifu vinavyotekelezwa dhidi ya mawakili.
Visa hivyo ni pamoja na mlipuko katika afisi ya mawakili ya IMMMA chini ya mwezi mmoja na tisho la waziri wa maswala ya kikatiba na sheria Harrison Mwakyembe la kutaka kufutilia mbali chama cha mawakili nchini Tanzania katika kipindi cha miezi saba iliopita.

No comments:

Post a Comment