Wednesday, October 4

Miji ya Sydney na Melbourne kukumbwa na joto kali miongo michache inayokuja

Beachgoers at Bondi Beach in SydneyHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMiji ya Sydney na Melbourne kukumbwa na joto la juu miongo michache inayokuja
Miji miwili mikubwa zaidi nchini Australia itakumbwa na joto la nyusi joto 50 miaka michache inayokuja , kwa mujbu wa utafiti.
Miji ya Sydney na Melbourne inatarajiwa kukumbwa na hali hiyo licha ya kasi ya kuongezeka kwa joto duniani kudhibitiwa na mkataba wa Paris wa kuzuia kuongezeka joto kwa viwango visivyozidi nyusi joto mbili
Kuzuia kuongezeka joto chini ya viwango hivyo kunaweza kuzui viwango hivyo kufika nyusi joto 50, kwa mujibu wa wanasayansi.
Mji wa Sydney ulifikia nyusi joto 45.8 mwaka 2013 huku Melbourne nao ukafika nyusi joto 46.4 mwaka 2009.
Utafiti huo ulitangazwa maeneo ya Victoria na New South Wales, lakiniawatafiuri wanasmeakwa semu zingien za Australia pia zitaathiriwa.
Kati ya miaka iliyokumbwa na joto la juu zaidi duniani ni mwaka 2015.
Mmoja wa watafiti Dr Lewis, alisema kuwa miji hiyo itashuhudia nyusi joto 50 kati ya mwaka 2040 na 2050.
Msimu wa joto wa hivi majuzi nchini Australia ulivunja rekodi 205 huku msimu wa baridi ukiwa wenye joto zaidi kwa mujibu wa baraza huru la hali ya hewa nchini humo.
Mwezi uliopita watu nchini Austalia walionywa kujiandaa kwa mto mkali wa nyika mwak 2017-2018.

No comments:

Post a Comment