Mkurugenzi wa kituo hicho Dinna Patrick alisema kuwa uwanja huo ungemalizika miaka sita iliyopita, lakini kutokana na mgogoro wa ardhi dhidi ya wananchi katika eneo ndio ulikwamisha ujenzi wa uwanja na kituo hicho.
“Baada ya kuwaomba wananchi kuwa eneo la uwanja huu utakuwa ni faida kwa watoto wetu, wakaamua kwa pamoja niendelee na ujenzi baada ya kikao cha wanakijiji na viongozi wa serikali za mtaa kisha wakaafikiana tujenge.”
Hata hivyo, viongozi wa kituo hicho wameamua kukarabati majengo mawili ya nyumba za kuishi walimu katika shule ya Julius Nyerere kwa ghalama ya Sh 30milioni, ikiwa kama shukrani kwa wananchi.
Uwanja huo ukimalizika unatarajia kuingiza watazamaji 15,000, huku ndani yake vikijengwa viwanja vingine vya mchezo wa kikapu, wavu, riadha, soka, pete, kuogelea, Ragbi, na kriketi.
No comments:
Post a Comment