Maafisa kutoka kote duniani wanakutana nchini Ufaransa kujaribu kutafuta njia za kuzuia kwa asislimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu ifikapo 2030.
Ugonjwa huo unasambaa kupitia maji machafu huwaua karibu watu 100,000 kila mwaka.
Ni mara ya kwanza serikali, shirika la afya duniani, mashirika ya misaada na wafadhili wametoa ahadi kama hiyo.
Hii inakuja wakati Yemen inandelea kupambana na moja ya milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu katika historia yake.
Ugonjwa wa Kipindu pindu katika karne ya 21 umeelezewa kama ''aibu kubwa kwa dunia,"
Ugonjwa huo ulitokomezwa nchini Uingereza na Marekani zaidi ya miaka 100 iliyopita , lakini unaendelea kusababisha vifo katika mataifa mengi yanayoendelea.
Si ghali kutibu ugonjwa huo na unaweza kuepukika kabisa ikiwa watu watapata maji safi na vyoo visafi.
Lengo kuu katika mkutano wa leo litakuwa ni maeneo yanayoathiriwa zaidi na kipindupindu barani Afrika na Asia, ambako milipuko hutokea mara kwa mara.
Maafisa hao wataahidi pia kumaliza milipuko inayowakumba watu wengi inayosababishwa na mizozo au majanga ya asili.
No comments:
Post a Comment