Marco Pellegri alipitisha mkono wake katika nywele zake na kuchukua simu yake iliokuwa katika mfuko wa ndani wa koti lake.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa akijizuia kutobubujikwa na machozi.
Lakini mwishowe alilazimika ,na alikaa katika kiti chake na kutokwa na machozi ya raha.
Pellegri amaye ndio msimamizi wa timu hiyo alikuwa amemuona mwanawe Pietro mwenye umri wa miaka 16 akifunga bao lake la kwanza na la pili kwa timu hiyo katika mechi ya ligi ya Serie A dhidi ya Lazio baada ya kuchukua mahala pake Ricardo Centurion katika kipindi cha kwanza.
Ilikuwa ndoto iliofanikiwa kwa babake mtoto huyo, Marco ambaye alikuwa akisema kwamba iwapo nitamuona Pietro akiichezea Genoa katika uwanja wa Luigi Ferraris atafurahi.
Atajihisi kana kwamba maisha yake yamekamilika.
Picha za Marcos akionekana akibubujikwa na machozi ziligonga vichwa vya habari duniani na zikamfanya Pietro kushindwa kujieleza alipoonyeshwa baada ya mechi ambapo Genoa ililazwa 3-2.
Na baadaye ilikuwa Pietro, saa alizokuwa ndani ya gari huku babake akimpeleka katika mechi moja hadi nyingine.
Mshambuliaji huyo mchanga pia naye alijawa na hisia.
Mwisho mazungumzo yalikuwa ya Petro kufunga mbele ya eneo la Gradinata Nord , eneo ambalo mashabiki wa Genoa hukongamana.
Wapellegri wanatoka Genoa.
Wanaishi Pegli, mji wa baharini uliopo magharibi ambapo Genoa ina uwanja wake wa soka.
Marco ameifanyia kazi klabu hiyo kwa miaka mingi, awali akiwa katika chuo cha mafunzo ya soka, na sasa akiwa mkufunzi wa Genoa.
Mkewe Marzia anatoka katika familia ya mashabiki wa Sampdoria.
Lakini Pietro amekuwa akiwaona wale wa Genoa pekee.
Wakati klabu hiyo iliposhushwa daraja hadi katika daraja la tatu kufuatia kashfa ya udanganyifu wa mechi miaka 12 iliopita ,Marco Rossi , nahodha wa klabu hiyo alikuwa akicheza playstation na mwana wa Pellegro.
Rossi aliichezea Genoa mara 286 na hadi leo amekuwa mfano mkubwa katika klabu hiyo. Pietro alipenda kuishabikia klabu moja pekee, Genoa.
Kitu kinachoweka historia ni kwamba licha ya kuwa kinda, klabu maarufu zimekuwa zikitaka kumsajili kwa miaka kadhaa.
Beppe Marotta, mkurugenzi wa Juventus , anadai kwamba alijaribu kumsajili Pietro miaka miwili iliopita wakati ambapo hakuna aliyemjua.
Msimu huu Inter Milan ilikubali kulipa Yuro milioni 60 kumsajili Pietro pamoja na kinda mwengine wa Genoa Eddie Salcedo, na ni sheria za Fifa za fair Play zilizozuia uhamisho huo.
Na kufikia siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, AC Milan ilitaka kumsajili Pietro baada ya kumuuza M'baye Niang.
''Lakini mpango huo haukufaulu'', alisema afisa mkuu mtendaji Marco Fassone.
Bado watajaribu tena.
Wengine wanasema ni mapema mno kubaini talanta ya kinda Pietro na kwamba dunia lazima iwe makini.
No comments:
Post a Comment