Tuesday, August 1

DC MNDEME AMPONGEZA MAVUNDE KWA KUTATUA KERO YA MAJI KWA WANANCHI WAKE




Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akiwa ameketi katika mmoja ya kaya za wakazi wa Mhande akipata chakula baada ya kuzindua mradi wa maji. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. 
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na akina mama wa kijiji cha Mhande 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akiteta jambo na Brother Anthony ambaye ni muasisi wa mradi wa CPPS. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akikagua eneo la pampu ya maji ya mradi wa maji wa Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akicheza ngoma baada ya kuzindua mradi wa maji 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhande 

……………………………………………………………..

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.

Mradi huu umetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya Ngh’ongh’ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa la upatikanaji maji safi na salama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero kubwa ya Maji katika kata ya Ngh’ongh’ona.

Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.

“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema

Hata hivyo amesema hatasita kuwachukulia hatua watu watakaoharibu miundombinu ya mradi huo wa maji huku akiwataka kuunda kamati ya maji ili kuendesha mradi huo.

Aidha amesema kwa kushirikiana na Mavunde watashughulikia upatikanaji wa umeme katika mradi huo wa maji ili uweze kutoa huduma ipasavyo kwa wananchi.

Naye, Diwani wa Kata hiyo Philipo Nangu amesema wananchi hao wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji na kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma hiyo vijiji jirani jambo lilosababisha kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Kadhalika, Mavunde amesema amefanikiwa kupata ufadhili wa Shirika la GIZ la Ujerumani ambao watasaidia kusambaza huduma hiyo ya maji katika kata yote ya Ngh’ong’hona ili kumaliza changamoto ya Maji kwenye eneo hilo.

No comments:

Post a Comment