Tuesday, August 1

MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA


Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.


Na fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang'ota wa kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika halmashauri hiyo.

"Ukiangalia hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili kukuza mapato ya halmashauri yetu"walisema madiwani

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua changamoto za Mji wa Mafinga.

"Angalieni nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya" walisema wananchi

No comments:

Post a Comment