Saturday, August 19

Seneta Chapelle - Nadal mashakani kwa kutaka Trump auawe

NadalHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionNadal anasema alikuwa na hasira alipoandika maoni hayo.
Seneta kutoka Missouri anachunguzwa na walinzi wa rais wa Marekani baada ya yeye kusema anatumai Rais Donald Trump atauawa.
Seneta huyo wa chama cha Democratic Maria Chappelle-Nadal alichapisha maoni hayo kwenye mtandao wa Facebook lakini baadaye akayafuta.
Walinzi wa rais wanasema "wanachunguzaa maoni yaliyotolewa na wengine" na kuwa "vitisho vyote dhidi ya Rais" vitafuatiliwa.
Seneta anakiri alikosea kwa kuandika hivyo kwenye Facebook lakini hatajiuzulu.
Aliandika "Hapana." Natumaini Trump atauawa!" wakati alikuwa anamjibu mtu kwenye Facebook.
Aliiambia St Louis Post-Dispatch: " Kwa hakika sikumaanisha kile nilichokiandika. Nimeiondoa, na ninadhani imefutwa.
"Sitajiuzulu. Nilichosema ni makosa, lakini sitakoma kuzungumzia kile kilichosababisha niseme hivyo, ambayo ni hasira na suitofahamu ambayo watu wengi nchini Amerika wanahisi sasa."
Wajumbe wa chama chake walikashifu maoni yake na wengine wametoa wito wa kujiuzulu kwake.
Kiongozi wa Democratic Caucus katika Seneti ya Missouri, Gina Walsh, alisema mwenzake "lazima awe na aibu kwa kuongeza sauti yake kwa yale yanayoendelea kwenye mazingira haya yenye sumu."
Seneta wa Democratic Claire McCaskill, ambaye pia ni wa Missouri, alisema: "Ninaushutumu, ni vibaya na hivyo lazima ajiuzulu."
Gavana wa Republican wa Missouri Eric Greitens amemwomba pia ajiuzulu.
Alisema: "Tunaweza kuwa na tofauti katika nchi yetu, lakini hakuna mtu anayepaswa kuchochea vurugu za kisiasa. Seneta lazima ajijiuzulu."
Hata hivyo, Seneta Chappelle-Nadal anasisitiza kuwa ana haki ya kuzungumza.
"Nimekataa kujiuzulu kwa kutumia haki yangu, hata kama nilivyosema ni makosa," alisema.

No comments:

Post a Comment