Saturday, August 12

Mwanamke Muislamu aliyevuliwa hijab na polisi alipwa $85,000

Kirsty PowellHaki miliki ya pichaCAIR
Image captionKirsty Powell
Mwanamke mmoja Muislamu ambaye alilazimishwa kuvua hijab yake na maafisa wa polisi mjini California amezawadiwa $85,000 (£65,000).
Kirsty Powell aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya baraza mji wa Long Beach baada ya kulazimishwa kuvua vazi lake la hijab kufuatia kukamatwa kwake 2015.
Ombi la Bi Powell la kutaka kuhudumiwa na afisa wa polisi mwanamke lilipuuzwa na akalazimika kulala jela bila hijab yake.
Idara hiyo sasa imebadili sera yake kuhusu mavazi ya kidini ya kichwani.
Maafisa wa kike sasa wanaruhusiwa kuondoa hijab zao mbali na maafisa wa kiume na wafungwa iwapo usalama wa maafisa hao unatishiwa, alisema jaji wa Long Beach Monte Machit akizungumza na gazeti la Los Angeles Times.
Hatahivyo baraza la mji wa Long Beach lilikubali kumaliza kesi hiyo kulingana na baraza la mahusiano ya waislamu .
Baraza hilo ambalo lilianzisha kesi hiyo lilisema kuwa maafisa wa polisi kwa lazima walivua hijab yake mwanamke huyo mbele ya maafisa wa polisi wanaume na makumi ya wafungwa.

No comments:

Post a Comment