Saturday, August 12

Trump atishia kuisababishia Korea Kaskazini "shida kubwa" kwa sababu ya Guam

Donald Trump na Mike Pence in Bedminster, New Jersey, on 10 August 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump amesema Kim Jong-un atajuta sana, na upesi sana, iwapo atatishia kisiwa cha Guam tena
Rais wa Marekani Donald Trump ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba nchi hiyo inafaa kutarajia shida kubwa, kubwa" iwapo kitu chochote kitatendeka kwa kisiwa cha Marekani cha Guam.
Akiongea akiwa Bedminister, New Jersey, aliahidi kwamba kisiwa hicho katika Bahari ya Pasifiki kitakuwa "salama kabisa, na mniamini".
Bw Trump amesema Marekani itaiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi, "vikali zaidi".
Baadaye alizungumza na Rais wa China Xi Jinping, ambaye alisisitiza umuhimu wa kutatua mzozo huo kwa njia ya amani, runinga ya serikali ya China ilisema.
Rais Xi alitoa wito kwa wahusika wote kuwa na subira na kujizuia dhidi ya kutoa maneno au kufanya vitendo ambavyo vinaweza vikazidisha uhasama.
Aidha, alisema ni kwa maslahi ya China na Marekani kwamba kusiwepo na silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.
Ikulu ya White House ilisema Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini ni lazima ikomeshe "tabia yake ya uchokozi na kuongeza uhasama."
"Twatumai kwamba mambo yatakuwa sawa," Bw trump alisema awali, akionekana kuwa na msimamo wa matumaini siku moja baada yake kuonekana kukata tamaa.
"Hakuna anayependa suluhu ya amani zaidi ya Rais Trump, hilo ninaweza kuwaambia."
Mapema Ijumaa, Trump alikuwa amesema jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule.
"Suluhu ya kijeshi sasa ipo, imepangwa na iko tayari, Korea Kaskazini wakidhubutu kuchukua hatua isiyo ya busara. Twatumai Kim Jong-un atachagua njia nyingine!" Trump ameandika kwenye Twitter.
Alisema hayo huku Korea Kaskazini ikimtuhumu kwa kukaribia kutumbukiza rasi ya Korea katika vita vya nyuklia.
Trump aliandamana na waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson (kushoto) na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley mjini Bedminster, New JerseyHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump aliandamana na waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson (kushoto) na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley mjini Bedminster, New Jersey
Pyongyang inakamilisha kuandaa mpango wake wa kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.
Urusi imesema majibizano kati ya Washington na Pyongyang yanafaa "kututia wasiwasi sana."
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema kiwango cha hatari ya kutokea mzozo wa kivita ipo "juu sana" huku akipendekeza mpango wa pamoja wa Urusi na China wa kutanzua mzozo huo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hakuna suluhu yoyote inayoweza kupatikana kupitia jeshi, na kwamba "kuongezeka kwa majibizano sio suluhu."
Alipoulizwa kuhusu tamko lake Ijumaa kwamba jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule, Trump aliwaambia wanahabari: "Natumai kwamba wanafahamu (Korea Kaskazini) uzito wa nilichokisema na nilikisema ndicho ninachokusudia...maneno hayo ni rahisi sana, rahisi sana kuyaelewa."
Aliongeza: "Iwapo yeye (Kim Jong-un) atatoa vitisho vyovyote zaidi hata kwa lugha fiche ... kuhusu kisiwa cha Guam au eneo jingine lolote ambalo ni la Marekani au mshirika wa Marekani, atajutia sana kwa kweli na atajutia hilo haraka sana."
Bw Trump ameandika hivyo kwenye Twitter baada ya kutishia mapema wiki hii kupitia Twitter kwamba "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Aidha, Ijumaa, shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini KCNA liliituhumu Marekani kwa "jaribio la kihalifu la kusababisha mkasa wa kinyuklia katika taifa hilo la rasi ya Korea."
Shirika hilo lilisema Marekani inafanya kila juhudi kufanyia majaribio silaha zake za nyuklia katika rasi ya Korea.
Marekani ndiyo "mpanga njama ya tishio hili la nyuklia, mraibu wa vita vya nyuklia," taarifa ya KCNA imesema.
Awali, alikuwa ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba inafaa kuwa na "wasiwasi sana" iwapo itatenda lolote kwa Marekani.
Alisema utawala wa taifa hilo utakuwa shida kubwa "ambayo ni mataifa machache sana yaliyowahi kukumbana nayo" iwapo "hawatabadilika".
Kadhalika Bw Trump alikuwa awali ameshutumu serikali za awali za Marekani akisema zilionyesha udhaifu sana zikikabiliana na Korea Kaskazini na pia akashutumu mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini, akisema kwamba inafaa "kufanya juhudi zaidi."
Alisema: "Nawaambia, iwapo Korea Kaskazini itafanya jambo lolote hata kwa kufikiria tu kuhusu kumshambulia mtu tunayempenda au tunayewakilisha au washirika wetu au sisi wenyewe inaweza kuwa na wasiwasi sana, sana."
"Nitawaambia ni kwa nini...ni kwa sababuu mambo yatawatendekea ambayo hawajawahi kufikirtia kwamba yanaweza kutokea."
Hata hivyo, aliongeza kwamba Marekani bado iko huru kushiriki katika mashauriano.
Aliongeza: "Nawaambia hivi, Korea Kaskazini inafaa kujiweka sawa au wataona shida kubwa kiasi ambacho ni nchi chache sana zilizowahi kushuhudia."
Andersen Air Force Base, Guam July 18, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani ina kambi ya jeshi la wanahewa la Andersen kisiwa cha Guam
Korea Kaskazini ilisema Jumatano kwamba inapanga kurusha makombora ya masafa wa wastani na ya masafa marefu kuelekea kisiwa cha Guam, ambapo kuna kambi ya ndege za kivita za kuangusha mabomu za Marekani.
Hata hivyo, kufikia sasa hakujakuwa na dalili zozote kwamba huenda kisiwa hicho cha Guam kikashambuliwa.
Map showing Guam

Kisiwa cha Guam na umuhimu wake

  • Kisiwa cha Guam kina ukubwa wa kilomita mraba 541 (maili mraba 209) na kinapatikana bahari ya Pasifiki kati ya Ufilipino na Hawaii.
  • Ni jimbo "lisilo na mpangilio wowote, na lisilojumuishwa kikamilifu" la Marekani, lenye wakazi karibu 163,000.
  • Kambi za jeshi la Marekani hutumia karibu robo ya ardhi ya kisiwa hicho. Marekani ina wanajeshi 6,000 kisiwa hicho na kuna mipango ya kuwasafirisha maelfu wengine huko.
  • Ni kituo muhimu katika shughuli za kijeshi za Marekani, ambapo huwezesha wanajeshi wa nchi hiyo kufika maeneo mengi muhimu Pasifiki, mfano eneo la bahari linalozozaniwa la South China Sea, rasi ya Korea na mlango wa bahari wa Taiwan.
Bw Trump alikuwa amewaambia wanahabari Jumanne kwamba: "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Seneta mkongwe wa Marekani John McCain hata hivyo alikuwa na shaka kuhusu tamko la Trump.
"Viongozi wengi wakuu ambao nimewahi kuwaona, huwa hawatoi vitisho ikiwa hawako tayari kuvitekeleza na sina uhakika kwamba Rais Trump yuko tayari kuchukua hatua," alisema Bw McCain.
Korea Kaskazini ilikuwa imeghadhabishwa na vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba "Marekani italipia" kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.
Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull amesema taifa lake liko tayari kushiriki katika vita dhidi ya Korea Kaskazini iwapo nchi hiyo ya rasi ya Korea itatekeleza shambulio dhidi ya Marekani.
"Iwapo kutakuwa na shambulio dhidi ya Marekani, Mkataba wa Anzus wa mwaka 1951 utaanza kutekelezwa na Australia itajitokeza kuisaidia Marekani," alisema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, "vile vile ambavyo Marekani ingefika kutusaidia iwapo tutashambuliwa."

No comments:

Post a Comment